ADA Estates, Kindondoni, Dar es salaam +255 745 805 805
info@bejez.co.tz

News

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA OFISI ZA  KAMPUNI YA SILENT OCEAN CHINA

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA OFISI ZA  KAMPUNI YA SILENT OCEAN CHINA

Akiendelea na ziara yake nchi  China aliyoianza jana, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, leo asubuhi alifungua rasmi ofisi za Kampuni ya Silent Ocean maarufu Simba wa Bahari, inayojishughulisha kusafirisha mizigo kutoka China kwenda Tanzania. 

Dk . Mwinyi amesema kuna biashara kubwa kati ya Tanzania na China na kwa kuifungua ofisi hiyo ushirikiano wa kibiashara utaongezeka zaidi baina ya nchi mbili hizo.

Pia amewahimiza wawekezaji wa China kuwekeza zaidi Zanzibar  na angependa Kampuni za China zije Tanzania  kuangalia fursa zaidi za kuwekeza. 

Akimkaribisha Rais Dk. Mwinyi kufungua rasmi kampuni hiyo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki amesema kufunguliwa kwa Kampuni ya Silent Ocean iwe ni chachu kwa Kampuni nyingine za Tanzania  kuendeleza ushirikiano  wa biashara na China.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Silent Ocean Bwana Salaah Said Mohamed amesema wanahudumia kupeleka mizigo kutoka China kwenda chi zore za Afrika Mashariki na Kati kwa miaka 19 sasa.

Alibainisha uwezo wa kampuni yake kuusafirisha makasha 600 hadi 1000 kwa mwezi na kupongeza uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Xi Jing Ping wa Jamhuri ya watu wa China kufungua njia  ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

🗓️ 28 Juni 2023

📍China.

Image

Office Address

  • 121 King Street, Australia
  • example@gmail.com
  • (00) 2500-123-4567

Social List